Psalms 89:29-34


29 aNitaudumisha uzao wake milele,
kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.


30 b“Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,

31 kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,

32 cnitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,

33 dlakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.

34 eMimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
Copyright information for SwhKC